MADAKTARI BINGWA KUTOKA DAE SES SALAAM WATOWEKA BILA TAARIFA KWA WAGONJWA MKOANI KATAVI,WAGONJWA WAHAHA KUPATA MATIBABU,MGANGA MKUU MKOA WA KATAVI ASHIKWA KIGUGUMIZI KUSEMA HALI ILIVYO-Agosti 18,2017
Mh.Anna Lupembe Mbunge viti Maalumu Katavi(PICHA na.Issack Gerald) |
Hali hiyo imeibuka
leo katika viwanja vya polisi Mpanda baada ya wagonjwa kuwasili katika viwanja
vya polisi tangu alfajili na hatimaye kutowaona madaktari wanaotakiwa kuwapima
na kuwatibu ambapo wameiomba serikali kuhakikisha madaktari wanajipanga kabla
ya kuja kutoa huduma.
Baadhi ya wagonjwa
wakiwa wamekata tamaa kutokana na hali kutoeleweka pamoja na mambo mengine
wakaeleza ya moyoni mwao.
Hata hivyo Kutokana
na hali hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Yahya Hussein amefika kutoa
ufafanuzi mbele ya wagonjwa zaidi ya 100 waliokuwepo ambapo hakutaka kurekodiwa
na chombo cha habari wakati akizungumza na hatimaye kusema chanzo cha madaktari
kuondoka ni uhaba wa dawa.
Jumanne ya Wiki hii
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu alizindua
zoezi la Siku tano la upimaji wa magonjwa Sugu ambapo juzi na jana akiwa
Wilayani Tanganyika na Mlele aliwahamasisha wakazi kujitokeza kwa wingi
kupatiwa matibabu.
Wakati
huo huo,mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe aliyekuwa
akiratibu zoezi zima la kuleta madaktari hao mkoani Katavi alipotafutwa kwa
njia mbalimbali ikiwemo kwa ya simu ili atoe ufafanuzi wa hali ilivyo juhudi
hazikufanikiwa hata simu yake licha ya kuwa hewani haikupokelewa ambapo hata
Mkurugenzi wa Taasisi ya CCP ya Dar es Salaam inayohusika na kudhibiti magonjwa
sugu Dkt.Frank Manase ambaye naye alikuwa akiongoza masafara wa madaktari
bingwa 25 naye pia hakupokea simu alipotafutwa
Miongoni mwa
magonjwa sugu yaliyokuwa yanapimwa na mengine kutibiwa ni pamoja magonjwa ya
moyo ikiwemo Shinikizo la damu na magonjwa ya saratani ikiwemo saratani ya
mlango wa shingo ya kizazi saratani ya matiti saratani ya tezi dume na ugonjwa
wa kisukari.
Jumla ya madaktari
bingwa 25 kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
taasisi ya Saratani ya Ocean Road na taasisi zinazoshghulikia matatizo ya meno
zilikuwepo kuendesha zoezi la siku tano la kupima na kutibu wagonjwa ambapo
hata hivyo wametumia siku tatu badala ya siku tano huku mamia ya wakazi mkoani
Katavi wakikosa kupimwa na kutibiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments