RC KATAVI ATAKA WATENDAJI WA VIJIJI KUWA NA DAFTARI LA WAKAZI-Agosti 9,2017
Mkuu wa Mkoa wa katavi
meja jenerali mstaafu Raphael
muhuga amewataka watendaji wote wa
vijiji mkoani hapa kuwa na daftari la
wakazi katika maeneo yao.
Ameyasema hayo katika
ziara yake mwishoni mwa wiki katika kijiji cha isengule na ikola wilayani
Tanganyika ambapo amesema kila mtendaji
wa wakijiji ahakikishe anakuwa na
daftari la kuandikishia wakazi ili kuepuka uhamiaji haramu katika mkoa wa
katavi.
Aidha muhuga amwasistiza
kwa kusema kuwa kufanya hivyo kutadumisha
ulinzi na usalama katika nchi kutokana na wahamiaji wengi kufanya
matukio na kutoweka.
Kumekuwa na wimbi kubwa
la wahamiaji haramu katika nchi ya Tanzania kutokana na baadhi yao kukimbia
vita na njaa katika nchi zao.
Comments