RTO KATAVI:WAMILIKI IMARISHENI MAGARI YENU KABLA YA SAFARI-Agosti 9,2017
Wamiliki wa magari katika halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda mkoani katavi wametakiwa kuhakikisha magari yao yanakuwa imara
kabla ya kuyaigiza barabarani.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa usalama
barabarani mkoani Katavi John Mfinanga wakati akizungumza kuhusu operesheni ya
ukaguzi wa magari ilianza kwa lengo la kuhakikisha magari yanakuwa imara na
salama kabla ya kuanza safari ili kuzuia ajali za barabarani.
Mfinanga amebainisha kuwa operesheni
hii ni endelevu na endapo watakamata magari mabovu hayataruhusiwa kusafirisha
abiria kwenda eneo lolote mpaka wamiliki wataka po yatengeneza .
Operesheni hii ni ya nchi nzima na
kwa mkoa wa dar salaam inajulika kwa jina la nati kwa nati wakati mkoa wa
katavi ikijulikana kwa jina la nati kwa boliti.
Comments