OPARESHENI BOMOABOMOA YAENDELEA KULIZAWAKAZI MKOANI KATAVI-Agosti 9,2017
WAKAZI wa
kitongoji cha Mgolokani Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba
serikali kurejeshewa ardhi yao au kuwatafutia maeneo ya kuweka familia zao
kufuatia kufukuzwa na nyumba zao kubomolewa ambapo serikali imedai kuwa wakazi
hao wanaishi ndani ya misitu ya hifadhi.
Wakazi hao
wakiwemo Bi.Grace Aloyce na Leonard Maembe,wakizungumza na Mpanda
Radio,wamesema mpaka sasa wanalala nje huku baadhi ya mali na vyakula vya familia
vikiwa vimepotea wakati wa oparesheni ya kubomoa makazi yao.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kitongoji cha Mkogokani Bw.Divason Kisulo,amesema wamekuwa
wakiishi katika eneo hilo tangu mwaka 1974 ambapo amesema zaidi ya kaya 200
zimebomolewa makazi yao na kusababisha zaidi ya watu 1, 075 kuathirika kwa
kukosa mahali pa kuweka familia zao pamoja na upotevu wa mali.
Hata hivyo
kutokana na kutompata mkuu wa Wilaya ya Mpanda ili kuzungumzia mgogoro huo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kusema hawezi
kulizungumzia suala hilo.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga akiwa
safarini,ameiambia Mpanda Radio kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Mpanda
atafuatilia uhalali wa eneo hilo.
Comments