SERIKALI YA MTAA MKOANI KATAVI YAHOFIA MAFURIKO YA WANAFUNZI-Agosti 12,2017
SERIKALI ya mtaa wa Kampuni kata ya
Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,Imeiomba Manispaa ya Mpanda kuandaa miundombinu
ya madarasa ya kutosha katika shule ya msingi Nsambwe,ili kukidhi idadi ya
wanafunzi itakayoongezeka katika shule hiyo baada ya wakazi wa mtaa wa msasani na
tambukareli kuhamia eneo hilo wakiwa na wanafunzi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kampuni
Bw.James Simon amesema,vyumba viwili vya madarasa vilivyopo katika shule ya
msingi Nsambwe haviendani na idadi ya wanafunzi takribani 300 waliopo huku
baadhi yao kati ya hao hulazimika kusomea nje.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati
ya shule ya msingi Nsambwe Bw.Joseph Mayala amesema Shule ya Msingi Nsambwe iliyoanzishwa
mwaka 2015 kwa sasa ina wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tano na walimu
watatu ambapo amesema kama hakuna vyumba vingine vya madarasa vitavyojengwa
hali itakuwa mbaya zaidi hasa msimu wa mvua.
Zaidi ya kaya 300 za mtaa wa Msasani
watakaobomolewa makazi yao na shirika la Reli Tanzania TRL ifikapo mwezi
Januari mwakani ili kupisha mipaka ya hifadhi ya reli Wilayani Mpanda
wanatarajia kuhamia katika mtaa wa kampuni hali itakayopelekea ongezeko la
idadai ya wanafunzi na kuleta changamoto
Comments