RAIS UHURU KENYATTA ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYA-Agosti 12,2017
Uhuru Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja |
wafuasi wa Jubilee wakifurahia kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama msahindi wa uchaguzi mkuu |
Rais
Kenyatta alipata kura 8, 203, 290.. ambayo ni asilimia 54 naye mpinzani wake
mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga
akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.
Akitangaza
matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati
alisema kuwa ni asilimia 78 ya wapiga kura milioni 19 waliosajiliwa pekee
walioshiriki katika shuguhuli hiyo ya kidemokrasia.
Alisema
kuwa licha ya matatizo machache kukumba mfumo mpya wa kutangazia matokeo, tume
yake ilifanikiwa kutangaza matokeo hayo bila tashwishi yoyote.
Aliongezea kuwa hatua
zilizochukuliwa kuandaa uchaguzi huo ni hakikisho tosha la ukomavu wa
kidemokrasia nchini.
Alisema
kuwa Wakenya wengi walijitokeza na kivumilia hali ya anga ili kushiriki katika
zoezi hilo la kidemokrasia kutokana na uaminifu walio nao kwa tume hiyo ya
uchaguzi.
Aliongezea
kwamba licha ya kukumbwa na changamoto chungu nzima katika mahakama waliweza
kuandaa uchaguzi huo kwa njia ya haki uwazi na uhuru,
Akitoa
hotuba yake rais Uhuru Kenyatta amewashukuru wafuasi wake na Wakenya wote kwa
jumla kwa kumpatia muhula mwengine.
Aidha amemtaka mpinzani wake mkuu Raila Odinga
na wafuasi wake kushirikiana naye katika kujenga Kenya akisema kuwa Uchaguzi
huja na kumalizika lakini wakenya ni sharti wasalie kama mandugu na majirani
wema.
Na muda mfupi tu baada ya
Uhuru Kenyatta kutanzwa rais mteule wafuasi wake kote nchini walisherehekea
ushindi huo kwa vifijo na nderemo.
Muungano
wa upinzani ulikuwa umepinga utaratibu uliokuwa unatumiwa na tume hiyo
kupeperusha matokeo ya uchaguzi huo.
Aidha,
viongozi wa muungano huo walikuwa wamedai mitambo ya tume hiyo ilidukuliwa na
matokeo kubadilishwa.
Viongozi hao walikuwa Alhamisi wametangaza
kwamba mgombea wao, Bw Odinga ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali
ya Mwai Kibaki, kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Comments