MADAI YA WAKAZI WA KITONGOJI CHA MGOLOKANI MKOANI KATAVI KUDAI KUWAMIWA NA SERIKALI NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAO WAKATI WA OPARESHENI YA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU KUWAKUTANISHA VIONGOZI WA WILAYA YA MPANDA KUSAKA SULUHU-Agosti 15,2017
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi ijumaa ya wiki hii,inatarajia kukutana na Uongozi wa Wilaya ya
Mpanda pamoja na viongozi wa hifadhi ya misitu Wilayani Mpanda, kujadili madai
ya wananchi wa kitongoji cha Mgolokani kilichopo kijiji cha Matandalani kata ya
Sitalike halmashauri ya Nsimbo wanaodai kuvamiwa na Serikali na kuharibu makazi
yao kwa madai yanayotolewa na serikali kuwa wakazi hao wamejenga makazi yao
katika eneo la hifadhi ya misitu.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Mh.Raphael Kalinga amebainisha hayo leo wakati akieleza hatua zinazochukuliwa
na Halmashauri ili kutafuta ufumbuzi wa madai ya wakazi wa kitongoji cha
Mgolokani wanaodai pia kuwa wapo nje ya mipaka ya hifadhi ambapo mpaka sasa
mamia ya wakazi kwa zaidi ya wiki moja tangu kubomolewa makazi yao wameendelea
kuishi chini ya miti.
Wiki iliyopita,mwenyekiti wa
kitongoji cha Mgolokani Bw.Divason Kisulo alisema mpaka sasa kaya zipatazo 215
zimebomolewa makazi ya yao na baadhi ya mali zao zikiwemo sola za umeme kupotea
wakati wa zoezi la ubomoaji ambapo wakazi wapatao zaidi ya 1075 wanatarajia
kuathirika ikiwa oparesheni katika eneo hilo litaendelea.
Wakati huo huo wakazi wa eneo hilo walidai
mtu mmoja alifariki dunia kwa kugongwa na gari na mwingine kujeruhiwa kwa kile
ambacho wananchi walidai kuwa walipatwa na ajaili hiyo katika harakati za
kubomoa makazi yao.
Wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wanadi
kuishi katika kitongoji hicho kuanzia mwaka 1974 ambapo mwezi Julai mwaka huu
2017 wahifadhi wa misitu walifika kuhakiki mipaka na wakazi hao kuhakikishiwa
kuwa wao wako eneo salama hali ambayo iliwaacha na mshangao nyumba zao
zilipoanza kubomolewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga amekuwa akisisitiza kuwa lazima waliojenga
ndani ya hifadhi katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mpanda lazima watii
agizo la kuondoka katika maeneo hayo.
Maeneo mengine ambayo yamekumbwa na
oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa kuvamia hifadhi za misitu hivi
karibuni ni kijiji cha Litapunga pamoja na Kitongoji cha Makutanio katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Habari zaidi Bofya www.p5tanzania.blogspot.com
Comments