WAZIRI WA AFYA MH.UMMY MWALIMU KUWASILI KESHO MKOANI KATAVI KUZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA-Agosti 15,2017
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu |
WAZIRI wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh.Ummy
Mwalimu anatarajia kuwasili kesho mkoani Katavi kwa ajili ya kuzindua zoezi la
siku tano la upimaji wa magonjwa
yasiyoambukiza.
Mbunge wa viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lupembe akizungumza na
waandishi wa habari katika viwanja vya polisi Mpanda amesema,timu ya madaktari
bingwa wapatao 25 kutoka Dar es Salaam kutoka taasisi mbalimbali wamewasili
Mkoani Katavi kwa ajili ya zoezi hilo.
Mkurugenzi wa taasisi ya kinga dhidi ya magonjwa sugu CCP Medicine ya
Dar es Salaam Dk.Frank Manase pamoja na mambo mengine amesema,katika zoezi hilo
lililoanza leo na kutarajiwa kufikia tamati Ijumaa ya wiki hii,wameambatana na
taasisi mbalimbali zikiwemo taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete,Taasisi ya saratani ya Ocean road,madaktari kutoka chama
cha kisukari Tanzania na taasisi ya
madaktari wa kinywa na meno na lengo likiwa ni kutoa huduma ya upimaji wa afya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahya Hussein
amesema,pamoja na ukosefu wa vifaa vya kupimia magonjwa sugu Mkoani Katavi pia Mkoa
wa Katavi una ukosefu wa madaktari bingwa wa magonjwa sugu ya wanaume huku
kukiwa na madaktari bigwa wawili pekee wanaopima magonjwa ya wanawake.
Miongoni mwa Magonjwa sugu yanayopimwa ni pamoja na magonjwa ya moyo
na saratani yakiwemo saratani shingo ya kizazi,kiharusi,shinikizo la damu la
juu,saratani ya matiti na saratani ya tezi dume ambapo sababu kuu ya kuongezeka
magonjwa hayo ni pamoja na tabia ya ulaji kutofanya mazoezi, kutokuwa desturi
ya kupima afya mara kwa mara na uvutaji wa sigara.
Habari zaidi
www.p5tanzania.blogspot.com
Barua pepea:p5tanzania@gmail.com,Mawasiliano 0764491096
Comments