MADEREVA BAJAJI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI WAGOMA,SUMATRA WATOA TAMKO KALI WASISITIZA HAKUNA BAJAJI KUPITA BARABARA KUU KUANZIA KESHO AGOSTI 8,2017
WAENDESHA pikipiki za tairi tatu
maarufu kama bajaji Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo wamegoma kutoa huduma
ya usafiri wakilalamikia hatua ya Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu
SUMATRA kuwazuia kutumia barabara kuu zinazotoka mpanda mjini na kusafirisha
abiria kupitia barabara kuu.
Akizungumza na waandishi wa habari
mbele ya mamia ya waenedsha bajaji kwa
niaba ya waendesha bajaji Mkoani Katavi,Bw.Rashid Juma amesema,mipaka ya
usafirishaji abiria ambayo imewekwa na Sumatra inawadidimiza kiuchumi kwa kuwa
wanategemea kuendesha maisha ya familia zao kutokana na vyombo hivyo vya
usafiri.
Kwa upande wake Afisa wa mamlaka ya
udhibiti wa usafiri wa majini na nchi Kavu Sumatra Mkoani Katavi Bw.Aman
Mwakalebela amesema kuanzia kesho Agosti 8 hakuna pikipiki aina ya bajaji
itakayoruhusiwa kutumia barabara hususani kutoka Mpanda mjini kupitia barabara
ya Sumbawanga na Kigoma.
Hata hivyo Naye mwenyekiti wa
usafirishaji Mkoani Katavi Nassoro Alfi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya
usalama barabarani Mkoani Katavi amekiri kupokea taarifa ya mgomo ambapo
ameshauri serikali itumie busara katika
suala hilo kutokana na kutokuwepo njia nyingine mbadala zitakazomwezesha dereva
wa babajaji kupita kumfikisha abiria mahali anatkotakiwa kufika.
Katika hatua nyingine kutokana na
mgomo wa madereva bajaji,baadhi ya wagonjwa,wajawazito wameshindwa kufika
katika vituo vya afya ambapo pia abiria na madereva wa bajaji wameelezea kuathiriwa
na mgomo huo.
Habarika zaidi na www.p5tanzania.blogspot.com
Comments