SHIRIKA LA INTERNATIONAL AID SERVICES LATOA MSAADA WA MAFUTA KWA AJILI YA WENYE ULEMAVU WA NGOZI-Agosti 8,2017
SHIRIKA la International Aid Services(IAS)
limetoa msaada wa mafuta yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa
ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ili kuzuia mionzi mikali ya jua inayochoma
ngozi zao.
Akizungumza jana kupitia kikao baina
ya shirikia hilo na kikundi cha walemavu na wazazi wa watoto wenye ulemavu, Mkurugenzi
wa shirika la IAS linalojishghulisha na kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu
katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Irene Shayo,amewataka watu wenye ulemavu
kushirikana katika matatizo pamoja na kutoa sauti ya pamoja kuhusu na matatizo
yanayowakabili.
Lakini pamoja na mambo mengine Irene
Shayo ameelezea jinsi shirika linavyofanya kazi ya kuibu watoto wenye ulemavu katika
mikoa miwili pekee Tanzania ya Katavi na Rukwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi wa shirika la IAS hapa nchni Bw.Jacksom Kaluzi amesema pamoja na shirika
la International Aid Services kuchangia shilingi laki moja katika mfuko wa
kikundi cha walemavu na wazazi wa watoto wenye ulemavu,amekitaka kikundi hicho kuibua
miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujiendeleza baada ya shirika hilo
kujiondoa katika ufadhili.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama 46
wa kikundi cha walemavu na wazazi wa watoto wenye ulemavu,mwenyekiti wa kikundi
hicho Bernard Nkana ambaye pia ni mwenyelkiti wa mtaa wa Mpadeco Kata ya
Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,amesema kwa upande wao kama
wanachama wanakusudia kuanzisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya kusaidia watoto
wenye ulemavu ili wakamilishe ndoto zao.
Baadhi ya wazazi wenye watoto wenye
ulemavu wamesema wanapata shida sana katika malezi hasa wanapokosa vifaa
saidizi kwa watoto wenye ulemavu.
Wakati huo Shirika limesema
linaendelea na mchakato wa kushughulikia baiskeli kwa ajili ya baadhi watu
wenye ulemavu pamoja na kushirikiana na serikali katika kutafuta ufumbuzi wa
matatizo yanayowaguza watoto wanaohitaji kupatiwa elimu kama watoto wasiokuwa
na ulemavu.
Shirika la International Aid
Services(IAS) linashirikiana na mashirika mengine ya Free Pentecostal Church Of
Tanzania(FPCT) na International Centre Of Disabilities(ICD) ambayo kwa pamoja
yanaunda umoja uitwao IFI
Comments