Pichani ni mjumuiko wa wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii wanaohudhuria warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro. Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye kazi za vikundi. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay akifungua warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Na.Mwandisi waetu-ARUSHA IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha,imepungua kufikia asilim...