RUKWA WAJIPANGA KUHIFADHI MAZINGIRA
NA.Issack Gerald-SUMBAWANGA
Mkoa wa Rukwa Umepanga kupanda miti milioni
Tano na laki tano katika Halmshauri zake kwa mwaka wa 2015/2016 lengo likiwa ni
kuhifadhi mazingira.
Hatua hiyo imeelezwa na Mshauri wa mazingira na maliasili Mkoani Rukwa Nichoraus Mchome wakati akizungumza na
Mpanda Radio Ofisini Kwake.
Aidha Mchome amesema kuwa katika
kuhakikisha usafi unadumishwa Mkoani humo hususani Manispaa ya Sumbawanga na maeneo mengine ya Mkoa wa Rukwa, imeteuliwa
siku ya Alhamisi kuwa siku ya Usafi Kimkoa.
Hata hivyo baadhi ya wakazi
wanaofanya usafi Manispaa ya Sumbawanga,wamesema wanafanya kazi katika
mazingira magumu huku wakitumia gharama zao kununulia vifaa vya kufanyia usafi huku
wakisema kuwawanafanya kazi hizo kutokana na kutokuwa na namna nyingine ya
kuendesha maisha ya kila siku.
Comments