WAKULIMA WAOMBA PEMBEJEO ZA KILIMO ZILETWE MAPEMA
Na. Lutakilwa Lutobeka-MPANDA
Kucheleweshwa
kwa pembejeo kwa wakulima imeelezwa kuwa ni sababu inayozorotesha sekta ya
kilimo wilayani Mpanda, mkoani Katavi.
Baadhi ya
wakulima wilayani Mpanda wamesema hayo wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Wamesema kuwa serikali imekuwa ikichelewesha pembejeo kama mbolea na mbegu
hivyo kushindwa kwenda sambamba na msimu wa kilimo.
Aidha wakulima hao
wameiomba serikali kuleta mapema pembejeo ili walime na kupata mazao
yanayoridhisha.
Naye Kaimu afisa
kilimo wa wilaya ya Mpanda Bw. Kennedy Nveramo amesema wamekwishapata pembejeo
kutoka mkoani na muda wowote wataanza kusambaza kwa wakulima.
Katika msimu wa
kilimo uliopita baadhi ya wakulima walilalamikia serikali kwa kutoa mbegu za
mahindi ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa na nyingine hazikuota.
Comments