ASKARI WA WANYAMAPORI KATAVI WALALAMIKIWA KWA UDHALILISHAJI WA RAIA NSIMBO
Na.Masoud
Mmanywa-Nsimbo
WAKAZI wa kijiji cha
Mtisi Kata ya Stalike wilayani Nsimbo mkoani Katavi, wamewalalamikia askari wa
Wanyamapori kwa kuwapiga na kuwajeruhi kwa madai ya kuwakuta wakilima katika
eneo la hifadhi ya msitu.
Wakizungumza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtisi, wamesema wamekuwa
wakisumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kuwapiga hadi kuwajeruhi na
kusababisha shughuli za kilimo ambazo ndiyo tegemeo la wakazi hao kutofanyika
na kuishi kwa wasiwasi.
Miongoni mwa watu
waliopigwa ni Bw. Salamo Kayange mkazi wa kijiji cha Mtisi.
Mwenyekiti wa kijiji
cha Mtisi Bw. Pius Tito Mwantepela amesema kuwa, baada ya matukio hayo ya
kupigwa kwa wakazi wa kijiji hicho serikali ya kijiji imeshawasiliana na ofisi
ya maliasili na wamekiri kufanya oparesheni katika maeneo ya hifadhi.
Amesema kuwa tatizo
hilo ni la muda mrefu na hadi sasa halijapatiwa ufumbuzi na kwamba kijiji hicho
kilishaandika maombi ya kupewa ardhi itakayotumika kwa kilimo, kwani kijiji
hicho kilichoanzishwa mwaka 1982, kina ufinyu wa ardhi kutokana na kupakana na
migodi pamoja na eneo la hifadhi.
Comments