WAFANYABIASHARA,WANUNUZI WAILALAMIKIA SERIKALI KUPANDISHA BEI YA BIDHAA
Na.Issack Gerald-MPANDA
BAADHI
ya Wanunuzi na wafanyabiashara wadogo wadogo wilayani Mpanda mkoani Katavi
wameilalamikia serikali kutokana na kupandisha bei za bidhaa nchini kiasi
kinachowafanya washindwe kuyamudu maisha yao.
Malalamiko
hayo yametolewa leo na wafanyabiashara wanunuzi wakati wakizungumza na mpanda
redio, kutokana na kuongezeka kwa viwango vya bei kwenye bidhaa hasa vyakula, na kudai kuwa itawafanya kuendelea
kuwa maskini kutokana na kipato chao kuwa cha chini.
Aidha
wameiomba serikali mpya iliyoingia madarakani kuangalia kipato cha mwananchi
mmoja mmoja na kupanga bei zinazolingana na kipato halisi cha Mtanzania.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za
jamii Bw. Ephraim Kwesigabo zinaonyesha
kuwa mfumko wa bei za bidhaa umeongezeka
hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 mwezi septemba mwaka huu.
Comments