MIL.80 ZATUMIKA KUSAIDIA KAYA 62 ZILIZOATHIRIWA NA MVUA,WAFANYABIASHARA NAO KUFANYIWA TATHMINI
Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
Zaidi ya Shilingi Milioni 80
zimetumika kuwasaidia wahanga wa mvua iliyombatana na upepo Mkali Oktoba mosi
mwaka huu.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kwa njia
ya Simu ,Mratibu wa maafa Mkoani Rukwa Bi.Aziza Ramadhani amesema ,tahmini
ambayo imefanyika, imeonesha Jumla ya Kayazipatazo 62 zimebainika kuathiliwa vibaya sana na mvua
hiyo.
Aidha amesema,tathmini inaendelea
kufanyika ili kuwalipa fidia wafanyabiashara ambao biashara zao zimeharibiwa na mvua hiyo ikiwemo
magunia zaidi ya 300 ya vyakula mbalimbali katika maeneo ya sokoni.
Mbali na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania
kutoa tahadhari ya mvua za Elinino za mwaka huu kila mara ,Bi.Aziza amewashauri
wakazi wa Mkoa wa Rukwa kupanda miti inayozunguka kuzuia upepo pamoja na
kutoziba mifereji inayopitisha maji kuepusha maji kupenya katika makazi ya
watu.
Comments