WAKAZI KATAVI WATAKIWA KUWA TAYARI KWA USAFI DESEMBA 9
Na.Issack Gerald-MPANDA.
WAKAZI Katika Mkoa wa Katavi
wametakiwa Kuwatayari Kushiriki Katika zoezi la Kufanya usafi wa Mazingira
litakalofanyika Nchi nzima December 9 Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Dr Ibrahingu Msengi wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kuhusu Maandalizi
ya Utekelezaji wa Zoezi hilo kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.
Katika Maagizo yake Rais Magufuli
amewaagiza wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Hamashauri zote
nchini Kufanya Maandalizi ya upatikanaji wa Vifaa vya utekelezaji wa kazi hiyo.
Comments