UONGOZI HOSPITALI YA WILAYA MPANDA WALALAMIKIWA KWA KUTOA HUDUMA DUNI KWA WAGONJWA
Na.Issack Gerald-MPANDA
BAADHI ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda
wameulalamikia uongozi wa hospital ya wilaya ya Mpanda kwa kutoa huduma isiyoridhisha.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA wamesema
huduma inayotolewa hospitalini hapo inacheleweshwa kumfikia mgonjwa.
Aidha wameiomba serikali kuweka mikakati ya
upatikanaji wa damu salama ili kuokoa
maisha ya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Wilaya ya Mpanda Dr.Naibu Mkongwa amesema
tatizo la ukosekanaji wa damu salama linatokana na wananchi kutokuwa na mwamko
wa utoaji damu ili kupungunza ukosefu wa damu.
Wakati huo huo ameiomba serikali
kuleta vifaa vya kutosha katika hospital hiyo kwani hospitali hiyo inakabiliwa na
uhaba mkubwa wa vifaa kama vile mipira
na dawa.
Comments