MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA POLISI
Na.Mwandishi wetu-Mwanza.
Mahakama
kuu kanda ya mwanza imetupilia pingamizi la polisi kuzuia
waombolezaji kufanya ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chadema
mkoa wa geita Afonce Mawazo aliyeuwawa nov.14 mwakahuu kwa kukatwa mapanga.
Uamuzi
huo umefikiwa leo majira ya saa tano asubuhi baada ya Jaji Lameki mlacha
kusikiliza kesi ya madai iliyo funguliwa na chadema dhidi ya polisi kuwanyima
kibali na kupiga marufuku mkusanyiko wa kuugama mwili wa Marehemu mawazo
jijijni Mwanza.
Akizungumza
na wananchi baada ya mahakama kutoa uaumzi huo Mwanasheria wa chadema John
Mallya amesema kuwa mahakama chini ya Jaji Mlacha imefutilia mbali katazo la
polisi kutoaga mwili huo kwasababu ya kipindupindu na usalama kuwa hoja hizo
hazina mashiko na kilichobaki ni kupeleka mahakamani nyarajka za kuomba ruhusa
ya kuuga mwili huo.
Aidha
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa baada ya masaa mawili
nyaraka hizo zitakuwa tayari na kupelekwa mahakamani tayari kwa maamzi ya
mahakama.
Comments