VYAKULA VYA KUTEMBEZA MITAANI VYAPIGWA MARUFUKU MPANDA


Na.Issack Gerald-MPANDA
HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda imepiga marufuku  uuzaji wa  vyakula vya kutembeza, kama vile uji, barafu, juice na vyakula vinavyouzwa katika maeneo yasiyo rasmi.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Bw. Vincent Kayombo  amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuepukana na magojwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Kwa upande wake Afisa afya wa manispaa ya mpanda Bw. Paschal Kweya amesema amepokea vizuri agizo hilo na kuwa atawajibika ipasavyo kuhakikisha linafuatwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA