RAIA WAPYA KAMBI YA KATUMBA WAENDELEA KUFURAHIA KUWA WATANZANIA
Na.Issack
Gerald-MPANDA
MKUU
wa makazi ya Katumba yaliyopo wilayani Nsimbo mkoani Katavi Bw. Athuman Igwe, amesema jumla ya wakimbizi
waishio katika wilaya hiyo ni elfu kumi na tisa elfu mia saba sabini na tatu,
na waliopata uraia ni sitini na mbili elfu huku walio na vyeti ni hamsini na
saba elfu.
Ametoa
takwimu hizo jana wakati akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA ofisini kwake. Amesema kuwa, walio na uraia wanaweza kwenda
mikoa yeyote kwa uhuru hapa nchini na kwa ambao hawajapata vyeti utaratibu
unafanyika.
Wakazi
wa kata ya Katumba kijiji cha Mnyaki wameelezea furaha yao tangu kupata uraia
wa Tanzania, na kuwaomba Watanzani kutoa ushirikiano kwao ili kuleta maendeleo
katika jamii.
Comments