WATENDAJI WALIOGOMA KUHUDHURIA KIKAO CHA MKURUGENZI WILAYA YA MPANDA KUKABILIWA NA ADHABU
Na.Issack Gerald-MPANDA
HALMASHAURI
ya wilaya ya Mpanda imeagiza kuchukuliwa hatua kwa watendaji wa kata na vijiji
walioshindwa kuhudhuria kikao cha kazi kilichoitishwa na mkurugenzi bila
taarifa.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
Bw. Estom Chang’a katika kikao cha maelekezo ya utekelezaji wa kazi za kutatua
kero za wananchi katika maeneo yao.
Kikao
hicho cha kazi kimewashirikisha watendaji wa kata mbali mbali wakiwemo maafisa
maendeleo ya jamii katika ngazi ya vijiji kutoka kata zote za halmashauri ya
wilaya ya Mpanda.
Comments