WAKAZI MPANDA WAASWA KUJENGA NYUMBA BORA KUJIKINGA NA MVUA ZA ELNINO
Na.Issack
Gerald-MPANDA
WAKAZI
wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, wameshauriwa kujenga nyumba bora ili
kuepukana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazosadikika kuwa za
elnino.
Ushauri
huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya
Mpanda Bw. Paza Mwamlima wakati akizungumza na viongozi mbali mbali, wakiwemo watendaji wa vijiji, wenyeviti wa
mitaa, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Amewataka
kila mmoja kwa nafasi yake awajibike kuhamasisha wananchi kuwa makini na kuwa
tiba ya elnino ni nyumba bora.
Wakati
huo huo, amewaomba wahandisi kujenga mitaro mitaro bora ya kupitisha maji ili
maji yawe na mwelekeo mzuri na kuepusha athari kwa watu.
Comments