WAZAZI,WALEZI KATAVI WAASWA KUWAPELEKA VIJANA WAO KATIKA VYUO KUPATA SOKO LA AJIRA
Na.Issack Gerald-MPANDA
WAZAZI na walezi
mkoani katavi wameshauriwa kuwapeleka vijana wao katika vyuo mbalimbali vya
mafunzo ya ufundi stadi VETA ili waweze
kupata elimu itakayowasaidia kuingia katika soko la ajira ikiwa pamoja na
kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo masomo yao.
Ushauri huo
umetolewa na na mgeni rasmi katika mahafali
ya 26 ya kuwaaga wafunzi wa chuo cha
VETA Mpanda Bw. Sebastian Kapufi ambaye pia ni mbunge wa mpanda mjini.
Amesema wazazi
wa mkoa wa katavi wanapaswa kuitambua na kuitumia fursa iliyopo ya kuwa na chuo
cha ufundi karibu yao kwa kuwasomesha vijana wao.
Aidha katika mahafali
hayo Bw. Kapufi ametoa shilingi milioni moja kama zawadi ya wahitimu
waliomaliza masomo yao katika fani mbalimbali chuoni hapo.
Comments