WATANZANIA WAISHIO NCHINI THAILANDA WACHAGUA VIONGOZI WAO
Watanzania waishio mjini Bangkok nchini Thailand wakipata chakula baada ya kufanya uchaguzi |
Na.Mwandishi.BANGKOK
Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand (TIT) imekutana na
kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo
mbalimbali.
Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika Novemba 7 katika Hoteli ya Amari
Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
TIT ilianzishwa mnano mwezi Aprili mwaka huu na inahusisha watanzania
mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya kazi nchini
Thailand.
Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi
ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha mwaka
mmoja:Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya,Makamu menyekiti Bw. Alois Ngonyani,Katibu:
Bw.Andrew Wajama,Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi,Mhazini: Bw.
Adolf Kigombola,Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile,Afisa
Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni,Afisa
Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth
Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na
anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Mawasilano ya viongozi wa Jumuiya
hiyo ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)
+66947230002/+66972494819
Comments