UKEKETAJI WA WANAWAKE WAPUNGUA LOLIONDO ARUSHA
Pichani ni mjumuiko wa wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii wanaohudhuria warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro. |
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye kazi za vikundi. |
Na.Mwandisi waetu-ARUSHA
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo
wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha,imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya
Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na
mwandishi wa habari kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya
ya Uzazi na Maadili.
Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga
wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya
jamii.
Aidha wajumbe katika warsha hiyo wajumbea wamesema
kuwa watoto hususani wa kike wamekuwa wakikosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Comments