WABUNGE WATEULE WA BUNGE LA TANZANIA KUANZA KUSAJILIWA LEO
Baadhi ya wabunge la Tanzania wakiangalia mandhali ukumbi bungeni Mjini Dodoma |
Na.Mwandishi wetu-DODOMA
Wabunge wateule wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wanatarajia kujisajili leo tayari kwa vikao muhimu vya kwanza vya
Bunge wiki ijayo.
Wakati wabunge hao wakianza kujisajili kuanzia kesho na kesho
kutwa, Jumatatu ijayo itakuwa ni siku ya kupeana maelekezo, kutembelea Ukumbi
wa Bunge na mikutano ya kamati za vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ofisi ya Bunge iliyotolewa wiki
iliyopita, Jumanne Novemba 17, itakuwa siku ya kuanza kwa kikao cha kwanza kwa
kusomwa Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge.
Aidha kikao hicho kitafuatiwa na uchaguzi wa Spika, Kiapo cha
Uaminifu na Kiapo cha Spika na kisha Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote.
Comments