WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAANZA MTIHANI WA MOCK KIKANDA
Na.Issack Gerald-MPANDA
WANAFUNZI wa kidato cha sita katika
Manispaa ya Mpanda wameanza kufanya mtihani wa mock.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA,Afisa
elimu idara ya elimu ya sekondari Bi.Lutungulu Eliya amesema pamoja na kufanya mtihani wa mock,wamejiandaa kufanya
vizuri katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Machi mwaka ujao.
Hata hivyo Bi.Eneliya amezitaja
chanamoto zinazowakabiri kuwa ni pamoja na ukosefu wa walimu wa masomo ya
hesabu kutokana na wanafunzi kuongezeka na kufikia 759 ambapo kati yao walio
wengi wanasoma masomo ya sayansi.
Wakati huo huo serikali imeombwa kuongeza vifaa
vya kutosha vya sayansi ili kupata wataalam watakaokuwa msaada kwa jamii.
Comments