VIONGOZI NGAZI YA CHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA MASLAHI YA UMMA
Na.Issack Gerald-NSIMBO
VIONGOZI wa ngazi ya chini wametakiwa kufanya kazi kwa maslahi
ya umma ili kuendana na Kasi ya Rais Dr Jonh Pombe Magufuli.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi
wa Kata ya Kapalala iliyoko Katika halmashauri ya Nsimbo Mkoani hapa wakati wakitoa maoni yao juu ya hotuba
iliyotolewa na Rais Magufuli bungeni.
Katika hotuba yake Kupitia Kikao cha
bunge la 11 Rais Dr John Pombe Magufuli amewataka watendaji wote wa umma kuacha
kufanya kazi kwa Mazoea ili Kutatua matatizo na Kero zinazowakabili wananchi.
Comments