WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WALIA NA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wakazi wa kata ya Makanyagio katika Manispaa
ya Mpanda Mkoani katavi wameiomba
mamlaka ya maji safi na salama Manispaa ya Mpanda kutafuta ufumbuzi wa kuondoa
kero ya kukosekana kwa maji safi na salama kwa wananchi hao.
Wakazi hao wametoa kauli hiyo kwa
nyakati tofauti wakati wakizungumza na P5
TANZANIA MEDIA na kusema imekuwa na
changamoto ya ukosefu wa maji kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa kero kwa
wananchi.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mamla ya
maji safi na salama manispaa ya mpanda Injinia Zachari Nyanda amekiri kuwepo
kwa tatizo hilo na kusema kuwa mamlaka inafanya jitihada za kubadilisha mabomba
chakavu katika maeneo yasiyo na maji.
Licha ya kuwa maeneo Maeneo mengi hayana
maji safi na salama katika Manispaa ya Mpanda mitaa ya Kachoma, Majengo A, Majengo
B na madini ni miongoni mwa mitaa
iliyoathiriwa zaidi na ukosefu wa maji.
Comments