KAKESE,MWAMKURU WATAHADHARISHWA KIPINDUPINDU WAASWA KUDUMISHA USAFI
Na.Issack
Gerald-MPANDA.
WANANCHI
wa Kata ya Kakese na Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
wametakiwa kuzingatia usafi ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa
kipindupindu.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Afisa Afya wa
kata ya Kakese na Mwamkulu Abel Joseph Paul amesema elimu imetolewa kwa wananchi wa kata hizo juu
ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia kanuni na taratibu za
usafi wa mwili, vyakula na mazingira.
Aidha
amesema pamoja na Wanafunzi katika kata za Kakese na Mwamkulu kuelimishwa juu
ya maambukizi ya ugonjwa huu, Walimu hawana budi kuhamasisha zaidi,
ukilinganisha na msimu huu wa Matunda
kama maembe.
Hata hivyo,Mkuu wa Wilaya ya MLele
Bw.Suleman Isaa Njiku,akizungumza leo wakazi wa Manispaa ya Mpanda wakati wa
uzinduzi wa matumizi ya vipimo au mizani katika biashara,amesisitiza kila Mkazi
Mkoani Katavi kuhakikisha usafi wa kutosha unafanyikaambapo amesema kuwa yeyote
amabaye atakutwa akiishi mazingira machafu atachukuliwa hatua kwa mjibu wa
sheria zinavyoelekeza.
Comments