UZINDUZI MATUMIZI YA MIZANI,TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI ZAASWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA VIPIMO HALALI KATIKA BIASHARA
Mmoja wa wakazi wa Mpanda akionesha kauli mbiu ya hapa kazi tu siku ya uzinduzi wa wakala wa vipimo katika viwanja vya soko la Buzogwe Manispaa ya Mpanda (PICHA na Issack Gerald) |
Baadhi ya wafanyabiashara katika uzinduzi wa matumizi ya vipimo(mizani) katika biashara (PICHA na Issack Gerald) |
Na.Issack Gerald-MPANDA
Taasisi binafsi na
serikali ziwemo taasisi za dini,na vyombo vya habari zimeaswa kuhamasisha jamii
kutambua matumizi ya mizani katika biashara ili kupata tija katika shughuli za
kiuchumi.
Wito huo umetolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Njiku wakati wa uzinduzi wa matumizi ya vipimo
halali katika biasaha katika soko la Buzogwe lililopo Manispaa ya Mpanda.
Kwa upande wa Mratibu
wa Prigram ya ukopeshaji mizani Mkoani Katavi Moses Ntungi na Irene John ambaye
ni Kaimu Meneja wa sehemu ya elimu,habari na Mawasiliano wameataka
wafanyabiashara na wakulima Mkoani Katavi Kutumia vipimo ili kuondokana na
umaskini.
Mkoa wa Katavi umekuwa
mkoa wa kwanza kupewa kipaumbele cha
uzinduzi wa uuzaji na ununuaji wa bidhaa kwa kutumia vipimo kutokana na kuwa na
sifa kubwa ya kuzalisha mazao mengi ya kibiashara na vyakula.
Comments