UONGOZI SOKO KUU MPANDA WAKANUSHA KUTOZA USHURU MARA MBILI,KUTO TOA RISITI NA UNYANYASAJI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Uongozi wa soko kuu lililopo Wilayani
Mpanda Mkoani Katavi umekanusha madai yaliyotolewa na wafanyabiashara wa soko hilo
kuhusu kutozwa ushuru mara mbili na wasimamizi wa soko hilo.
Hayo yamebainishwa leo na mwenyekiti
wa soko bwana Aman Mahela wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA wakisema kuwa
hajawahi kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mfanyabiashara yeyote kuhusu kutozwa
ushuru mara mbili na kutopewa stakabadhi.
Hata hivyo Bw.Mahela amesema ikiwa wafanyabiashara watafanyiwa vitendo
hivyo ni vyema wakatoa taarifa mapema kwake ili madai hayo yashughulikiwe kwa
wakati.
Wiki mbili zilizopita wafanyabiashara
wa soko kuu la mpanda waliulalamika uongozi pamoja na wasimamizi wa soko hilo
kwa kuwatoza ushurru mara mbili pamoja na kutowakatia stakabadhi.
Comments