MKURUGENZI APEWA AGIZO KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA BUZOGWE
Na.Issack Gerald-MPANDA
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amepewa siku moja kuhakikisha anafika soko
la Buzogwe kuchunguza changamoto za ukosefu wa umeme,ulinzi wa biashara na maji
zinazowakabili wafanyabiashara waliopo katika soko hilo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Njiku kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Katavi,baada ya kupokea taarifa ya changamoto za wafanyabiashara wa
soko la buzogwe kutoka mwenyekiti wa Soko hilo Bw.Ramadhani Kalata.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa soko hilo Bw.Ramadhani Kalata amesema licha ya kutoa
ushuru wa Shilingi laki moja na themanini kwa kila mfanyabiashara kila
mwaka,wamekuwa wakikosa mazingira safi ya kufanyia biashara na huduma nyingine
zikiwemo umeme na maji.
Kwa
upande wa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamezu ngumza na P5 TANZANIA MEDIA
wamesema kuwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusiana na Changamoto zinazowakabili
sokoni hapo zitafanyiwa utatuzi.
Wfanyabiashara
hao wamezitaja changamoto zilizopo sokoni hapo kuwa ni Ukosefu wa huduma ya
maji,umeme,kutozwa ushuru ambao Rais Dr.John Magufuli alisema umefutwa sambamba
na kukosekana kwa ulinzi wa bidhaa zao hali inayopelekea wizi dhidi ya mali zao
kutokea.
Comments