MGOGORO WA WAFANYABIASAHARA WA MATUNDA SOKO LA MPANDA HOTEL WAMALIZIKA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wafanyabiasahara wa matunda katika
soko la Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda,wamewapongeza viongozi wa
Manispaa,madiwani , maafisa masoko na Bibi afya kwa kuwaruhusu kuuza matunda yao katika eneo
wanalolitaka baada ya kufanya usafi wa kuridhisha.
Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara
hao wakati wakizungumza na Mpanda Radio sokoni hapo.
Katika hatua nyingine wamesema kuwa,mgogoro
wa wafanyabiashara hao uliokuwepo kati yao na Mwenyekiti wa Soko hilo
Bw.Boniface Mganyasi wa kumtaka ajiudhuru umetatuliwa.
Novemba 17 mwaka huu,wafanyabiasahara
hao wa matunda waligoma kuondoka katika soko hilo wakidai kuwa haaiwezekani
kuondoka katika soko hilo kwa kuwa soko hilo wanalitegemea kuendesha maisha yao
na kusomesha watoto.
Comments