KATA YA SITALIKE KUKUSANYA MAPATO KUTOKA MIGODINI NA HIFADHINI
Na.Issack
Gerald-NSIMBO
UONGOZI
wa Kata ya Sitalike wilayani Nsimbo mkoani Katavi, unatarajia kukusanya mapato
kutoka kwa wawekezaji wa migodi pamoja na hifadhi ya taifa ili kuchangia
maendeleo ya kata hiyo.
Diwani
mteule wa Kata hiyo Bw. Adam Galamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na
Mpanda redio, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha Mtisi.
Bw.
Galamila amesema katika kata ya Sitalike kuna migodi mingi ya wawekezaji pamoja
na hifadhi ya taifa, ambayo kama michango yao itatumika vizuri kata hiyo
itapiga hatua kimaendeleo.
Aidha,
amesema mgogoro wa ardhi uliopo baina ya wakazi wa kata hiyo na hifadhi ya
taifa unaendelea kutafutiwa ufumbuzi ili wakazi wa kata hiyo waweze kufanya
shughuli za kilimo.
Comments