SPIKA BUNGE LA TANZANIA KUCHAGULIWA KESHO,SITTA NJE KINYANG'ANYIRO
Jengo la Bunge Mjini Dodoma |
Na.Mwandishi wetu-DODOMA
Wabunge wateule wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wanatarajia kumchagua Spika wa Bunge hilo kesho Mjini Dodoma.
Taarifa zinazoonesha ,wagombea uspika wasio wabunge, vyama
vingi vya siasa vimepeleka majina Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupitishwa.
Wakati huo huo Ratiba inaonesha kuwa kuanzia saa 10 jioni ya
leo, wabunge watakuwa na mikutano ya vyama vyao, ambapo hoja kubwa ni kuhusu
upatikanaji wa jina la Spika na Naibu Spika wake.
Tayari Chama cha Mapinduzi CCM kimeendelea na mchujo wa
majina ambapo jana kimewapitisha Naibu Spika wa Bunge la Kumi Job Ndugai,Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Dk. Tulia Akson na
AbdullahAllyMwinyi wakati huo jina la Spika wa zamani Samwel Sitta na wengine yakikatwa.
AbdullahAllyMwinyi wakati huo jina la Spika wa zamani Samwel Sitta na wengine yakikatwa.
Comments