WAKAZI KATAVI WAHIMIZWA USAFI
Na.Issack Gerald-MPANDA.
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa
kuzingatia usafi wa Mwili Mazingira na Vyakula ili kujikinga na Maambukizi ya
ugonjwa wa kipindupindu.
Wito huo umetolewa na Kaimu afisa
Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Noah Pius wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Amesema jamii inatakiwa kunywa maji
safi na salama yaliyochemshwa na kuchujwa pamoja na kuyahifadhi katika chombo
kisafi.
Aidha amesema wameunda kamati ya afya
ya Wilaya kwa ajili ya kutembelea maeneo
yote yanayozunguka Halmashauri hiyo kukutana na kamati za afya za vijiji pamoja
na kata ili kuhamasisha jamii kuzingatia usafi.
Comments