HALMASSHAURI YA MJI NJOMBE YAWAONYA WALIMU WAKUU WATAKAOFELISHA WANAFUNZI
Na.Mwandishi
wetu-NJOMBE
Halmashauri
ya mji wa njombe imesema itaendelea kutoa adhabu za kuwa vua vyeo walimu wakuu
ambao shule zao zinafelisha wananfunzi kuufikia wastani waliojiwekea ili
kukuhakikisha halmashauri hiyo inangara kielimu kwa kufikia ufaulu wa juu.
Afisa
elimu msingi wa halmashauri hiyo zegeli shengeli amesema kuwa kwa mitihani ya
darasa la saba mwaka huu halmashauri hiyo imeongeza ufaulu amapo kwa mwaka jana
zaidi ya shule 15 zililikua chini ya ufaulu lakini kwa sasa shule 5 pekee
zimeshindwa kuvuka ufaulu unaotakiwa
Amesema
kuwa miongoni mwa adhabu zinazotolewa kwa wakuu ambao wameshindwa kufaulisha ni
pamoja na kuvuliwa vyeo na kuhamishwa ili wajifunze na kwama kufanya hivyo
kumezaa matunda kwa shule nyingi kufanya vizuri
Shule
ya msingi Itipula ni miongoni mwa shule zilizofanya vibaya katika mtihani wa
darasa la saba kwa kushika nafasi ya mwisho kati ya shule 78 ambapo afisa elimu
amebainisha kuwa miongoni mwa sababu za kuanguka kielimu ni kukosekana kwa
ushirikiano baina ya walimu na kamati na wazazi
Kwa
upande wake mkuu wa shule ya itipula Ogorino ngoitanile amekiambia kituo hiki
kuwa tatizo la kufeli kwa wanafunzi shuleni hapo linatokana na wazazi
waliowengi kuwa na watoto wengi ambao wanashindwa kumudu kuwasomesha hivyo kuwa
shawishi kufanya vibaya mitihani ili kukwepa majukumu ya kuwasomesha wakifaulu
Wazazi
wa wananfunzi shule ya msingi itipula wamekiri kuwa chanzo cha wanafunzi kufeli
mitihani kwa madai kuwa kumekuwa na adhi yao huwafuata walimu na kuwatishia
pindi wanapo toa adhabu kwa watoto wanao feli masomo na hivyo kupelekea walimu
kukata tamaa ya kufeli
Pia
wameshauri serikali kuwachukulia hatua kali wazazi wenye tabia ya kuwatishia
wazazi ili kuleta maendeleo ya taaluma katika shule yao
Comments