MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA WAZIRI MKUU WA 11 TANZANIA TANGU UHURU WA TANGANYIKA
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza katika mkutano wa kwanza wa bunge la 11 kumchagua Waziri mkuu wa Tanzania na Naibu Spika |
Na.Mwandishi wetu-DODOMA
Mh. Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351 zilizopigwa, baada
ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye aliyekuwa
amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Waziri Mkuu.
Bw Majaliwa(55) mbali na kuwa amekuwa
mbunge wa jimbo la Ruangwa na Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
tangu 2010 pia alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali ya Mitaa.
Waziri Majaliwa
anatarajia kuapishwa kesho katika ikulu ya Dodoma.
Comments