WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA NI NANI?SOMA HAPA


 
Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu mteule wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alizaliwa Disemba 22, 1960 Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

 Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mnacho kati ya mwaka 1970-1976 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Kigonsera kati ya mwaka 1977- 1980.
Mwaka 1991-1993 alijiunga na Chuo Cha Ualimu Mtwara. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1994 na kuhitimu mwaka 1998 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden kwa masomo ya juu.
Amehudumu katika nafasi mbalimbali tangu mwaka 1984 alipojiunga na utumishi wa umma kama mwalimu mkoani Lindi, Katibu wa Chama cha Waalimu Wilaya, Katibu chama waalimu Mkoa na Mkuu wa Wilaya.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kabla ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumteua mwaka 2012 kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA