VIJANA MPANDA WAELEZA WALIVYONUFAIKA NA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI
Vijana katika kongamano Mjini Dodoma katika maadhimisho siku ya vijana Duniani |
Na.Issack Gerald-MPANDA
Vijana katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda walioshiriki
kongamano la wiki ya Vijana Oktoba 14 mwaka huu,wamesema kuwa walinufaika sana
na mafunzo mbalimbali ambayo wanatarajia kuyatumia na kufanikiwa katika
shughuli za kijasiliamali.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
baadhi ya vijana Mussa Jonasi Katuka na Hamis Abdul wamesema miongoni mwa
masuala amabyo walijifunza ni pamoja na usindikaji wa bidhaa,ufungashaji wa
bidhaa,namna ya kutafuta masoko ya bidhaa na umuhimu wa kuwa katika vikundi ili
kupata mikopo ya kuendeleza shughuli zao.
Kwa upande wake Fadhiri Secha amabye ni Afisa vijana
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda amesema kuwa,Halmshauri imejipanga kuwasimamia
vijana au makundi yaliyosajiliwa kisheria kwa ajili ya kuyapatia mikopo ya
kuendeleza shuguli ambazo wamezibuni.
Aidha,vijana na vikundi vya ujasiliamali vimetakiwa
kufuatilia habari mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mitandao kwa
ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kufanya kwa ajili ya kuondokana na
umaskini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ina Jumala ya vikundi 156 vya
ujasiliamali ambapo kuanzia mwezi Julai hadi Nvemba mwaka huu vikundi vya
wajasiliamali vipatavyo 20 vimepatiwa mikopo ambapo chanzo cha fedha ya mkopo
ni asilimia tano(5%) ambayo hutengwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmshauri
ya Wilaya ya Mpanda.
Kutengwa kwa asailimia 5% kwa ajili ya mkopo ni agizo la
serikali kuu ya Tanzania kwa Halmshauri zote hapa nchini.
Maadhimisho ya wiki ya vijana duniani yalifanyika Oktoba 14
mwaka huu huko mkoani Dodoma ambapo kama ilivyo kawaida hutanguliwa na
kongamano linaloanza Oktoba 8 na shrehe hizi ziliambatana na kumbukumbu ya kifo
cha Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru.
Comments