DAWA ZA MAGONJWA YASIYOKUWA YANAPEWA KIPAUMBELE KUANZA KUGAWIWA KESHO KATAVI
Na.Issack Gerald-MPANDA.
JAMII
Mkoani Katavi imetakiwa kuzingatia utaratibu wa wataalamu wa afya juu ya
matumizi ya dawa za magonjwa yasiyokuwa yanapewa kipaumbele Mkoani hapa.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Mratibu wa
Magonjwa hayo Mkoani Katavi Furahisha
Chaula amesema kesho wanatarajia kuanza zoezi la ugawaji wa dawa za majonjwa
ya Ngili maji, Trakoma, Usubi ,Minyoo na
Kichocho.
Amesema
kuwa mtumiaji wa dawa hizo anatakiwa kula na kushiba kabla ya kutumia dawa hizo.
Aidha
amesema kuwa dawa hizo ni salama, isipokuwa baadhi zinamaudhi madogo madogo yanayoweza
kujitokeza ikiwemo maumivu ya kichwa,tumbo na kichefuchefu.
Zoezi
hilo la ugawaji wa dawa utakaoanza kesho Desemba Mosi linatajiwa kumalizika desemba 05
mwaka huu.
Comments