WAKAZI MKOANI KATAVI WANAOZUNGUKA HIFADHI WATAKIWA KUTOFANYA SHUGHULI YOYOTE HIFADHINI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wananchi wanaoishi karibu na hifadhi
mbalimbali Mkoani Katavi wameshauriwa kutofanya
shughuli yoyote ndani ya hifadhi pamoja na
kuzingatia sheria ya uhifadhi ili
kuendelela kuzilinda hifadhi hizo.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa
hifadhi za misitu Wilayani Mpanda Mpanda Bw. Michael Kimata wakati akizungumza
na mpanda radio kuhusu ufafanuzi wa sheria ya uhifadhi pamoja na shughuli
zinazokataliwa kufanywa ndani ya hifadhi.
Amesema wananchi wanapaswa kutambua
kuwa jukumu la kulinda hifadhi siyo la
wahifadhi pekee bali ni wananchi wote wanaoishi jirani na hifadhi.
Aidha Bw. Kimata amesema wananchi wakishiriki
kulinda hifadhi na kuheshimu sheria za uhifadhi kutasaidia kuondoa migogoro
mingi ambayo imekuwa ikijitokeza kati ya wahifadhi na wanaovunja sheria hizo.
Comments