WAFANYABIASHARA WA MATUNDA SOKO LA MPANDA HOTELI WANAOUZIA CHINI WAGOMA KUOANDOKA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wafanyabiashara wa bidhaa katika soko
la Mpanda hoteil lililopo halmashauri ya mji Mpanda wamegomea agizo
lililotolewa na Mwenyekiti wa soko hilo bwana Boniphace Mganyasi la kutaka
kuhamisha bidhaa zao chini na kupeleka katika vichanja vya ndani.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa hii leo
katika soko la mpanda hoteil wakati wafanyabiashara wakipinga kwa nguvu zote
kuondolelwa katika eneo ambalo wamekuwa wakiweka biashara zao hususan
maembe,hukuwakisema ya kuwa mwenyekiti huyo amekuwa na upendeleo kwa baadhi ya
wafanyabiashara.
Kwa upande
wake bwana Dismas Benjamin ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara katika soko
hilo amesema serikali inabidi iwaangalie vizuri kutokana na wao kutegemea
biashara hiyo kusomesha watoto pamoja na kulea familia zao.
Akijibu tuhuma hizo
bwana mganyasi amesema kuwa yeye alikuwa anatoa taarifa tu kwa wafanyabiashara
kwani kuanzia kesho kutakuwa na na opresheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote
walio weka biashara zao chini.
Hata hivyo
wafanyabiashara hao walienda mbali zaidi na kumtaka mwenyekiti huyo ajiuzuru
lakini kabla ya kujiuzuru ni lazima wajue mapato na matumizi kwa miaka minne iliyopita.
Comments