KUUWAWA BODABODA KATAVI,KWAWAAMSHA POLISI KATAVI,WAAMUA KUITISHA MKUTANO WA BODABODA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya
mauaji ya waendesha pikipiki Mkoani Katavi,Mkuu wa usalama barabarani ameitisha
kikao kinachotarajia kufanyika kesho kujadili kwa kina suala hilo.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake,Mkuu wa Usalama Barabarani
Bw.Mafinanga John wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake.
Kwa upande wa waendesha bodaboda
Wilayani Mpanda wameelezea kufurahishwa na kuunga mkono hatua hiyo ya
Jeshi la polisi kufanya Mkutano kujadili changamoto za waendesha Bodaboda.
Naye Kaimu katibu wa chama cha
waendesha pikipiki Wilayani Mpanda,John Simtowe,amesema hatua hiyo ya polisi
kuitisha mkutano huo utazaa matunda kutokana na kuwepo wigo mpana wa kujadili
chanamoto zinazowakabili waendesha bodaboda hususani suala la mauaji.
Wiki iliyopita,mwendesha pikipiki
mmoja mkazi wa mtaa wa kichangani amekufa baada ya kuuwawa baada ya kuchukuliwa
na bodaboda huyo kumsafirisha kama abiria ambapo hata hivyo muuaji
hajafahamika.
Comments