WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI
Na.Issack Gerald-MPANDA
WATU
Wawili wanaokabiliwa na mashtaka ya kukamatwa na nyara za serikali,
wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda na kusomewa mashtaka.
Hakimu
Mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Bw. Adira Amworo, amewataja washtakiwa
hao kuwa ni Jastin Bruno mkazi wa Tompolo na Philbert Leo Uliza mkazi wa Ikuba.
Watuhumiwa
hao walikamatwa na polisi tarehe 17 mwezi huu katika Kitongoji cha Tompola
Kijiji cha Usevya Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi
wakiwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni
60,.
Kesi
hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tarehe 23 mwezi huu, na washtakiwa
wamerudishwa rumande.
Comments