Posts

Showing posts from May, 2016

AHUKUMIWA JERA MIEZI 6 KWA KOSA LA WIZI MPANDA

Mahakama ya mwanzo mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja mkazi wa Nsemlwa kifungo cha miezi 6 jera au kulipa faini kiasi cha shilingi laki mbili na nusu   kwa kosa la wizi kinyume na kifungu cha sheria namba 265 sura 16 kanuni ya adhabu.

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

WATU wawili wakazi wa Makanyagio wamefikishwa katika mahakama ya wilaya   ya Mpanda   kwa kosa la ubakaji.

KILICHOMKUTA MAKAMU MKUU WA SHULE MKOANI KATAVI AKITUHUMIWA KULAWITI WANAFUNZI WAKE

MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.

WANUSURIKA KIFUNGO JELA,MIFUGO YAO YATAIFISHWA MKOANI KATAVI

MAHAKAMA ya mkoa wa Katavi imetaifisha ng’ombe 1,312 walioingizwa na kuchunga ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa huku washtakiwa watatu wakinusurika kutumikia vifungo vya miaka miwili jela baada ya kulipa faini kati ya Sh 500,000 na 700,000.

WALIMU MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVIWAMEIOMBA SERIKALI KUWAPANDISHA VYEO WANAPOKUWA WAMEKIDHI VIGEZO.

WALIMU wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapandisha cheo wanapokuwa wamekidhi vigezo pamoja na kutengenezewa vitambulisho vipya   vya kazi.

WATU 5 WAKIWEMO WATATU WENYE KADI 19 ZA ATM ZA BENKI WANASWA NA JESHI LA POLISI KATAVI

WATU watatu wakazi wa tarafa ya kashaulili wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na kadi za ATM 19 za watu tofauti.

WIZI WAENDELEA KULINDIMA MPANDA WAHUSIKA MAHAKAMA YAENDELEA KUFANYA KAZI YAKE KWA WATUHUMIWA

MAHAKAMA ya mwanzo mjini Mpanda mkoani Katavi   inamshikilia   mtu mmoja kwa kosa la wizi wa mfugo wenye thamani ya shilingi elfu arobaini na tano.

VIONGOZI SERIKALI ZA VIJIJI WILAYANI MPANDA WATAKIWA KUTOKIUKA SHERIA ZA UGAWAJI WA ARDHI

VIONGOZI wa serikali za   vijiji wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kutokiuka   utaratibu wa kisheria katika ugawaji wa ardhi kwa wannchi.

MALIASILI KATAVI WATUHUMIWA KUTEKETEZA ZAIDI YAN NYUMBA 40 NA MALI ZA RAIA ZILIZOKUWA NDANI

KAYA zaidi ya 40 zimechomwa moto   na mali zilizokuwa ndani Katika kijiji cha Misanga Kata ya Tongwe Halmashauri ya Tanganyika   na watu wanaosadikika   kuwa ni maliasiri.

HAKIMU MFAWIDHI MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA ATOA WITO KWA WAKAZI MKOANI KATAVI KUEPUKA KUFANYA VITENDO UHARIFU

WANANCHI Mkoani Katavi wametakiwa kutofanya vitendo vya uhalifu ili kuepuka   madhara ambayo yatapelekea   kufungwa endapo   watabainika na makosa.

WANAWAKE WANAOUZA MIILI YAO MPANDA WATAKIWA KUFIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA KUPATA MBINU YA UJASILIAMALI KUEPUKA MAZINGIRA HATARISHI WALIYONAYO

WANAWAKE   Wanaofanya biashara ya Kuuza Miili yao   Maarufu kama (Dada poa) Mjini Mpanda   wametakiwa Kufika Katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ili Wapatiwe Mbinu za Kuunda Vikundi Vitakavyowawezesha Kuinua Uchumi ili kuwawezesha   Kuachana na biashara hiyo.

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA SIMU MPANDA

MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini   Mpanda    kwa   Kosa     la wizi wa simu   zenye thamani ya shilingi laki tatu.

SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU MAKAZI MAPYA YA KATUMBA MKOANI KATAVI

Raia wapya wa Tanzania wanaoishi Katika Makazi ya Katumba wanatarajia Kufanya Uchaguzi wa Viongozi wa   Serikali za Mitaa Mwaka huu ikiwa Mandalizi yameanza Kufanyika.

SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU HALMASHAURI YA WILAYA MPIMBWE MKOANI KATAVI

Serikali imesema kuwa imetenga kiasi cha shilingi milioni 246 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara za Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe zenye urefu wa KM 42 kwa kiwango changalawe kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

DIWANI NA MWENYEKITI WA KIJIJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WATAKIWA KUACHA TOFAUTI ZAO ZA KISIASA,WAANDISHI WA HABARI KUFUKUZWA MKUTANO WA HADHARA WANANCHI WANG'AKA

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imewataka Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw Makalai Njile na Diwani wa Kata ya ibindi Mh, Justin   Shinje Kuachana na Chuki za Kisiasa na badala yake wafanye kazi ya kutatua kero za wananchi wao.

DUKA LATEKETEA KWA MOTO MPANDA,ZIMAMOTO WAENDELEA NA UCHUNGUZI WA CHANZO

DUKA moja limeteketea kwa moto na kuungua baadhi ya bidhaa zilizokuwemo ndani katika maeneo ya soko la Mpanda hoteli mkoani Katavi.

KIKOSI CHA JADI KIJIJI CHA KAWANZIGE MPANDA CHAAPISHWA KUAPMABANA NA UHARIFU

KIKOSI cha ulinzi wa jeshi la jadi maalufu kama sungusungu katika kijiji cha Kawanzige kata ya Kakese manispaa ya Mpanda kimeapa kuendelea na mapambano dhidi ya uhalifu katika eneo hilo.

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA USIKU WA KUAMKIA LEO MEI 21,LAPITISHA WATUMISHI 13 KATI YA 16 WALIOKUWA WAMESIMAMISHWA KAZI KUKATWA MISHAHARA KUFIDIA HASARA ILIYOTOKANA NA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MIRADI ZA MANISPAA,MMOJA AFUKUZWA KAZI,WENGINE WATUPIWA TAMISEMI IWAPANGIE INAKOTAKA MBALI NA MANISPAA

Baraza la madiwani katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,limepitisha maamuzi   ya kukata mshahara wa watumishi 13 kati ya 16,waliokuwa wamesimamishwa kazi na baraza hiloFebruari 26 mwaka huu,kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwemo utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa taka pamoja na ubadhilifu wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese ambapo pia watumishi watatu wameshushwa vyeo.

PEMBEJEO ZA RUZUKU MSIMU WA KILIMO 2015/2016 ILIKUWA CHANGAMOTO TUPU KWA WAKULIMA MANISPAA YA MPANDA

WAKATI msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 ukitarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu,ripoti ya matumizi ya pembejeo Katika msimu uliopita wa 2015/2016 katika Manispaa ya Mpanda imeonesha kuwa ilitumia jumla ya pembejeo 27813 kati ya 32145 zilizoletwa katika Manispaa hiyo zimetumika.

WIZI WA SHUKA,GODORO NA FEDHA VYAMFIKISHA MAHAKAMANI MPANDA

Mtu mmoja mkazi wa kata ya Nsemulwa Wilayani Mpanda amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda kwa kosa la wizi wenye vitu vyenye thamani ya kiasi cha zaidi   ya shilingi laki tatu.

MBUNGE JIMBO LA MPANDA VIJIJINI ALINDIMA BUNGENI DODOMA KUTETEA VITUO VYA AFYA JIMBONI KWAKE

VITUO vya afya vya Mwese,Karema na Mishamo Wilayani Mpanda Vinakabiliwa na ukosefu wa wataalaamu wa afya na gari la wagonjwa-leo Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini Mh.Suleiman Kakoso alindima bungeni kutetea vituo hivyo.

RIPOTI KAMILI YA TUHUMA ZA MENO YA TEMBO: MCHUNGAJI KANISA LA MORAVIAN WILAYANI MLELE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE ZAIDI YA SHILINGI MIL.90

MCHUNGAJI wa kanisa la Moravian wilaya ya mlele  mkoni Katavi Gonweli Siame amefikishwa mahakamani katika mahakama ya hakimu mkazi  mkoa wa katavi kwa kosa la uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani zaidi ya million 90.

DIWANI KATA YA KATUMBA WILAYANI MPANDA KIZIMBANI KWA RUSHWA YA ZAIDI YA SHILINGI MIL.1

TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU  mkoa wa Katavi imemfikisha kizimbani  diwani wa kata ya Katumba  kwa kosa la kujihususha na vitendo vya rushwa.

JIONEE HII KALI: WAKAZI MTAA WA MSASANI MANISPAA YA MPANDA WATESWA NA KUNGUNI,WAOMBA SERIKALI IWASAIDIE DAWA YA KUWAUA

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wakazi wa Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwasaidia kupatikana dawa ya kuua wadudu aina ya KUNGUNI ambapo walisema kuwa wameshindwa kupata hata usingizi usiku.                                              

BREAKING NEWS :WANNE MBARON MPANDA KWA UKIUKWAJI BEI ELEKEZI YA SUKARI

WAKATI Serikali ikiendelea kupambana na watu wanaoficha sukari manispaa ya Mpanda mkoani katavi   imewakamata wafanyabiashara 4   ambao wanakiuka bei elekezi ya serikali ya kuuza sukari.

MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA APEWA SIKU 14 NA MKUU WA WILAYA YA MPANDA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI MISUNKUMILO

MKUU wa wilaya ya Mpanda Mh,Paza Mwamlima ametoa siku 14 Kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Kutatua Mgogoro wa aridhi kwa wananchi wa kata ya Minsunkumilo.

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3 KUTUMIKA KUJENGA HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI

SERIKALI ya mkoani katavi imeazimia   kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya    kuanzisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.

HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA YAZINDUA MNADA MPYA WA BULAMATA,ULINZI KUIMARISHWA SIKU ZA MNADA

Image
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda   Mkoani Katavi imezindua Mnada mpya wa mifugo wa Bulamata uliopo kata ya Bulamata ambapo pia bidhaa tofauti na mifugo zinatarajiwa kuuzwa katika mnada huo. Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)                             Afisa Mifugo Halmshjauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Bulamata  na maeneo jirani wakati wa uzinduzi wa Mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) Ng'ombe wakiwa mnadani siku ya uzinduzi wa a wa BulamataMnad(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) Mmoja wa wapishi katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) Mama akitengeneza kitoweo cha wateja  katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)...

RIPOTI KAMILI YA TAKUKURU MKOANI KATAVI KUWABULUZA MAHAKAMANI WATU WATATU KATI YA WATANO HII HAPA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Katavi TAKUKURU imewafikisha watu watatu katika mahakama ya wilaya ya   Mpanda kwa kosa la uhujumu uchumi.

WANANCHI WILAYANI MLELE WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA CHF

Image
WANANCHI katika kata ya Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani katavi wametakiwa kuwa mabalozi katika maeneo mbalimbali katika uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya CHF.                                                      

WATUHUMIWA WAWILI KATAVI AKIWEMO MCHUNGAJI KANISA LA MORAVIAN MBARONI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO YAKIWA YAMEHIFADHIWA KANISANI.

JESHI la Polisi mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo mchungaji wa kanisa la Moravian Usevya mkoani Katavi kwa kosa la kukutwa na vipande 11 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogram 20.3.

VIKUNDI 4 KATI YA 28 VYA WAJASILIAMALIVILIVYOPO KATA YA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI VIMEKABIDHIWA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 1 KUTOKA MFUKO WA JIMBO WA MBUNGE WA JIMBO LA MPANDA MJINI.

Vikundi 4 kati ya 28 vya wajasiliamali vilivyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo vimekabidhiwa mkopo kwa Shilingi milioni Moja kwa ajili kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

IDADI YA WATUMISHI HEWA YAZIDI KUPANDA KATAVI KUTOA 21 MWEZI ULIPOITA SASA 46 SERIKALI YAPATA HASARA ZAIDI YA MILIONI 200,MKUU WA MKOA WA KATAVI ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI KUWAFUKUZA KAZI WATUMISHI HEWA

IDADI ya Watumishi hewa Mkoani Katavi imeongezeka Kutoka 21 ya awali na kufikia watumishi hewa 46 walioisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 200,792,448.

SHILINGI MIL.1 YA MKOPO YATOLEWA NA MBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI KWA VIKUNDI 4 VYA WAJASILIAMALI KATA YA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA

Vikundi 4 kati ya 28 vya wajasiliamali vilivyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo vimekabidhiwa mkopo kwa Shilingi milioni Moja kwa ajili kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

WALIMU WAGOMA KUFUNDISHA WAKIPINGA MWALIMU MWENZAO KUPIGWA NA AFISA ELIMU,CWT KUTOA TAMKO LEO

WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.

WANAKIJIJI KASOKOLA MKOANI KATAVI WAKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI,KUSOMWA UPYA MEI 12 MWAKA HUU.

Wananchi wa kijiji cha kasokola kata ya kasokola manispaa ya mpanda wameikataa taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa   katika mkutano wa hadhara ambapo haijasomwa takribani mwaka mmoja na miezi mine.

WIKI YA WAUGUZI MKOANI KATAVI YAZINDULIWA WAGONJWA KUPATIWA MATIBABU BILA MALIPO HADI MEI 12 KILELE CHA MAADHIMISHO

WAUGUZI na Madaktari Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametiwa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kupuuzia maneno na vitendo vya watu wanaowakatisha tamaa ya kufanya kazi za utoaji huduma ya afya kwa ufanisi.

BODI YA CHAMA CHA MSINGI CHA USHIRIKA MPANDA KATI YAVUNJWA

BODI ya chama cha msingi cha ushirika cha wakulima wa tumbaku maarufu kama Mpanda Kati imevunjwa.