WANUSURIKA KIFUNGO JELA,MIFUGO YAO YATAIFISHWA MKOANI KATAVI
MAHAKAMA
ya mkoa wa Katavi imetaifisha ng’ombe 1,312 walioingizwa na kuchunga ndani ya
hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa huku washtakiwa watatu wakinusurika kutumikia
vifungo vya miaka miwili jela baada ya kulipa faini kati ya Sh 500,000 na
700,000.
Katika
shauri la kwanza mfugaji,Shigera Mayunga (22) amenusurika kifungo cha miaka
miwili jela baada ya kulipa faini ya Sh 700,000 katika Mahakama ya mkoa wa
Katavi huku ikimwachia kwa masharti mdogo wake, mwenye umri wa miaka 12 .
Washtakiwa
hao wawili walitiwa hatiani na mahakama hiyo kwa makosa ya kuingiza ng’ombe 532
na kuchungia ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa.
Hakimu
Odira Amworo akitoa hukumu hiyo pia aliamuru kutaifishwa kwa ngo’mbe wote 532
na kusema kuwa amelazimika kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wafugaji
wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali
Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali Achiles Mulisa alisema washtakiwa hao
wawili walitenda makosa hayo Machi , 2016 ambapo kwa pamoja waliingiza mifugo
yao na kuchunga ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa kinyume cha sheria.
Katika
shauri la pili wafugaji wawili, Ngusa Keleja “Mtungi” na Charles Mtokambali
(40) wamenusurika kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kila mmoja
wao kulipa faini ya Sh 500,000 kwa kuingiza ng’ombe 780 na kuchunga ndani ya
hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa .
Akitoa
hukumu hiyo,Hakimu Amworo pia aliamuru kutaifishwa kwa ng’ombe wote 780 na kuwa
amelazimika kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wafugaji wengine wenye tabia
kama hiyo.
Awali
Mwendesha Mashtaka,Wakili wa Serikali ,Mulisa alisema washtakiwa hao wawili
walitenda makosa hayo Machi 25, 2016 ambapo kwa pamoja waliingiza mifugo yao na
kuchunga ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Rukwa kinyume cha Sheria.
Kwa hisani ya gazeti la
Habari leo mei 29
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Comments