KILICHOMKUTA MAKAMU MKUU WA SHULE MKOANI KATAVI AKITUHUMIWA KULAWITI WANAFUNZI WAKE
MAKAMU
Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele
, Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Katavi
kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.
Mshtakiwa
huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga
Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya
dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani.
Mwendesha
Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa
mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba
2015 na Aprili 2016.
Alieleza
mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi
wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni
26 , mwaka huu litakapotajwa tena.
Inadaiwa
kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo
kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo
kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi
wake.
Kufuatia
msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi, Everest Hinju
na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani Mlele, Evaristo Kiwale
kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza na wanafunzi hao.
Wanafunzi
hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu
mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo. Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale alisema vitendo vya ushoga
havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika
vyombo vya kisheria.
Kwa hisani ya gazeti la
Habari leo mei 29
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Comments